MAJINA YA WADAHILIWA KATIKA AWAMU YA PILI

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ilitangaza kukamilisha kuchakata majina ya waombaji wa awamu ya pili tarehe 23/09/2018 na kuwa majina hayo yamekwisha rudishwa vyuoni kwa ajili ya kutangazwa. 

Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo SUA hatujaweza kutangaza majina yote ya waombaji waliochaguliwa katika awamu ya pili. SUA inaendelea kufanyia kazi suala hilo ikishirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania  na likikamilika muda wowote majina yatatangazwa. 

Tunaomba uvumilivu katika wakati huu mara tutakapo tatua changamoto iliyojitokeza majina yatatangazwa.

Mwisho tunaomba radhi tena kwa usumbufu uliojitokeza.

IMETOLEWA NA MKURUGENZI, 
KURUGENZI YA MASOMO YA SHAHADA ZA AWALI

Like & Share this page