TANGAZO LA MAFUNZO YA UFUGAJI BORA WA KUKU KWA MUDA MFUPI (WIKI MOJA)

Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) kwa niaba ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) inapenda kuwatangazia kuwa, kutakuwa na mafunzo ya muda mfupi (wiki moja) ya ufugaji bora wa kuku. Mafunzo hayo yatafanyika katika Ukumbi wa Giraffe uliopo katika Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) Kampasi ya Edward Moringe – SUA, Morogoro kuanzia tarehe 29.01.2024 hadi 01.02.2024. Walengwa, idadi ya waombaji na idara itakayotoa mada imeoneshwa kwenye Kielelezo Na. 1.

Share this page