NAMBA YA KOTESHENI: PA/012/2019-2020/HQ/W/22
KWA AJILI YA: HUDUMA YA KUWAPATA MAFUNDI WA KUFANYA UKARABATI WA MAJENGO MBALIMBALI YA OFISI, NYUMBA ZA WANYAMA NA UTAFITI KAMPASI KUU YA SUA
MWALIKO WA KOTESHENI
1.Mwaliko huu wa Kotesheni (MK) unafuata Tangazo la Jumla la Ununuzi (TJU) kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa mwaka 2019/2020 wa fedha baada ya kufanyiwa mapitio.
2.Serikali ya Tanzania imetenga fedha kwa ajili ya uendeshaji wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo katika mwaka wa fedha 2019/2020. Inakusudiwa kuwa sehemu ya fedha hizo itatumika kugharimia malipo halali chini ya mkataba ambao unatolewa katika huu Mwaliko wa Kotesheni (Zabuni Ndogondogo).
3.Unakaribishwa kuleta Kotesheni yako ya bei kwa ajili ya utekelezaji wa kazi kama ilivyoelezwa kwenye Mchanganuo wa Makadirio ya Kazi (MMK) kama ilivyofafanuliwa katika sehemu ya II ya nyaraka hizi.
4.Waombaji wote wanaweza kupata Kabrasha la Kotensheni hii katika Ofisi ya Afisa Mkuu Ununuzi na Ugavi, Jengo la Utawala, Kampasi Kuu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.
5.Kotesheni zote katika uhalisia wake (original) pamoja na nakala [moja] zinazofanana, zilizojazwa kwa usahihi na kuwekwa kwenye bahasha isiyo na maandishi juu na kuandikwa “Kotesheni Na. PA/012/2019-2020/HQ/W/22, Kundi Na….., ‘’HUDUMA YA KUWAPATA MAFUNDI WA KUFANYA UKARABATI WA MAJENGO MBALIMBALI YA OFISI, NYUMBA ZA WANYAMA NA UTAFITI KAMPASI KUU YA SUA’’. Ni lazima zipelekwe kwa;
Ofisi ya Afisa Mkuu Ununuzi na Ugavi,
Jengo la Utawala, Kampasi Kuu
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
S.L.P 3000
SUA MOROGORO
6. Waombaji wote wanatakiwa kuhudhuria kikao maalumu (Pre-bid meeting) tarehe 1/6/2020 siku ya Jumatatu saa 3:00 asubuhi, jengo la Utawala la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Kampasi Kuu ili wapate nafasi ya kutembelea na kuoneshwa maeneo yote yanayohusika katika Ukarabati huo kwa mujibu wa Mwaliko wa Kotesheni hii.
7. Siku ya mwisho ya kuwasilisha Kotesheni ni Jumatano tarehe 03 Juni, 2020 kabla ya Saa 8:00 Mchana. Kotesheni zitafunguliwa hadharani mara tu baada ya muda wa mwisho wa kuwasilisha, mbele ya wawakilishi wa wazabuni wanaoamua kuhudhuria katika ufunguzi wa zabuni katika;
Ukumbi wa Mikutano, Ghorofa ya Pili, Jengo la Utawala
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
S.L.P 3028,
SUA MOROGORO.
8. Kotesheni zitakazochelewa na kotesheni za kielektroniki hazitakubaliwa kwa ajili ya kutathminiwa kwa hali yoyote ile.
MAKAMU MKUU WA CHUO
CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA)
MOROGORO
Bofya hapa kusoma Tangazo la Zabuni (pdf)