Kesho tarehe 06/04/2018 ni siku ya uzinduzi rasmi wa wiki ya upandaji miti hapa SUA. Mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Japhet Hasunga. Uzinduzi utafanyika eneo la jirani na mabweni ya Nicolaus Kuhanga Kampasi Kuu ya SUA. Wote tunakaribishwa kuhudhuria shughuli hii muhimu na kushiriki kupanda miti. Ratiba inaanza saa 1:30 asubuhi. Ninaambatanisha ratiba ya siku nzima ya kesho.
RATIBA YA UZINDUZI WA WIKI YA UPANDAJI MICHE YA MITI SIKU YA IJUMAA, TAREHE 06/04/2018 ENEO LA JIRANI NA MABWENI YA NICOLAUS KUHANGA, KAMPASI KUU, SUA
MUDA |
TUKIO |
MHUSIKA/WAHUSIKA |
1.30 – 2.30 ASUBUHI |
WANAJUMUIYA WA KAMPASI KUU NA SOLOMONI MAHLANGU KUCHUKULIWA NA MAGARI KWENDA ENEO LA UPANDAJI MITI |
KAMATI YA MAANDALIZI, PPRO, WANAJUMUIYA YA CHUO |
2.30 – 2.45 ASUBUHI |
MGENI RASMI KUWASILI NA KUTIA SAINI KITABU CHA WAGENI OFISINI KWA VC |
MGENI RASMI, VC, DVC (AD), DVC (A&F), PPRO, RASI WA NDAKI YA MISITU, WANYAMAPORI NA UTALII |
2.45 – 3.00 ASUBUHI |
MGENI RASMI KUELEKEA ENEO LA UZINDUZI JIRANI NA MABWENI YA NICOLAUS KUHANGA
|
MGENI RASMI, VC, DVC (AD), DVC (A&F), PPRO, RASI WA NDAKI YA MISITU, WANYAMAPORI NA UTALII |
3.00 – 3.10 ASUBUHI |
MGENI RASMI KUPATA MAELEZO KUHUSU UPANDAJI MITI |
RASI WA NDAKI YA MISITU, WANYAMAPORI NA UTALII |
3.10 – 3.20 ASUBUHI |
MAKAMU WA MKUU WA CHUO KUMKARIBISHA MGENI RASMI AZINDUE RASMI UPANDAJI MITI |
MAKAMU WA MKUU WA CHUO |
3.20 – 3.30 ASUBUHI |
MGENI RASMI, WANAJUMUIYA WA SUA NA WAALIKWA WOTE KUPANDA MITI |
WOTE |
3.30 – 3.50 ASUBUHI |
MGENI RASMI KUZUNGUMZA NA WANAJUMUIYA WA SUA NA WAALIKWA WOTE |
MGENI RASMI |
3.50 – 4.00 ASUBUHI |
VIBURUDISHO NA MGENI RASMI KUONDOKA |
WOTE |
4.00 – 6.00 MCHANA |
WANAJUMUIYA WA SUA NA WAALIKWA WOTE KUENDELEA KUPANDA MITI |
WANAJUMUIYA YA CHUO NA WAALIKWA WOTE |
IMETAYARISHWA NA KAMATI YA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA UPANDAJI MICHE YA MITI - SUA