Siku ya Jumatatu, tarehe 31/12/2018 mbele ya Jengo kuu la Utawala katika eneo rasmi la Bendera hapa Kampasi Kuu ya Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kulifanyika hafla fupi ya kupandishwa rasmi kwa Bendera yetu ya Chuo ambapo Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa ni Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Raphael T. Chibunda.
Bendera ya Chuo(kushoto) ikiwa imepandishwa rasmi kwa mara ya kwanza na inaonekana sambamba na Bendera ya Taifa katika eneo la bendera kampasi kuu SUA.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA, wakishuhudia tukio adhimu la kupandishwa kwa mara ya kwanza Bendera ya Chuo lililoongozwa na Makamu wa Mkuu wa Chuo Jumatatu Desemba 31, 2018
Askari wa Usalama wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA, wakitoa heshima wakati wa upandishwaji wa mara ya kwanza kwa bendera ya Chuo Jumatatu Desemba 31, 2018. Katikati mstari wa mbele ni mgeni rasmi wakati wa tukio hilo, Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda. Tukio hilo limefanyika SUA, kampasi Kuu Morogoro.
Tunatoa pongezi kubwa sana kwa Menejimenti na Baraza la Chuo kwa hatimaye kufanikisha upatikanaji wa Bendera ya Chuo.
Imewasilishwa na,
Ofisi ya Mawasiliano na Masoko- SUA'