Matokeo ya Utafiti ya Mradi wa FoodLAND Kusaidia Kuboresha Kilimo na Lishe Afrika.

Imeelezwa kuwa matokeo yote mazuri ya Mradi wa Chakula Kilimo na Lishe (FOODLAND) yaliyopatikana kwenye nchi zinazotekeleza mradi huo yatakwenda kuisaidia jamii katika kuhusanisha Kilimo, Matumzi ya mazao ya chakula na lishe na hivyo kupunguza changamoto za chakula na lishe Afrika.

 

Matokeo ya Utafiti ya Mradi wa FoodLAND Kusaidia Kuboresha Kilimo na Lishe Afrika.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)  upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala wakati akifungua Mkutano Mkuu wa wa tatu wa Mwaka wa Mradi huo uliofanyika visiwani Zanzibar wa kufanya tathimini ya kazi zilizofanyika ndani ya mradi ili kuendelea kuboresha ufanyaji kazi wa mradi huo.

“Mradi huu unaunganisha kwanza uzalishaji wa chakula lakini pia na matumizi ya chakula kwa sababu kumekuwa na miradi mingi ambayo imekuwa ikiangalia  uzalishaji tu pekee na miradi mengine mingi ikiangalia matumizi ya chakula pekee kwa hiyo kunakuwa hakuna muunganiko au uhusiano kati ya uzalishaji na matumizi ya  chakula. Inawezekana chakula kinazalishwa sana kuliko kinavyoliwa au kinacholiwa zaidi si kinachozalishwa kwa kiwango kile ambacho kinahitajika”, alisema Prof Mwatawala.

1 (6) 0Naibu Makamu Mkuu wa Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)  upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala wakati akifungua Mkutano Mkuu wa wa tatu wa Mwaka wa Mradi huo uliofanyika visiwani Zanzibar.

Prof. Mwatawala amesema amefurahishwa sana na Mchanganyiko wa wadau wanaotekeleza mradi huo kwa kuwa unawahusisha Watafiti, Wajasiriamali na Wabunifu maana mwisho wa utafiti matokeo hayo yatawahusu watu hao katika makundi yao na watatakiwa kufanya kazi zao kwa kuzingatia matokeo yatakayopatikana kwakuwa ndio njia ya kufikia mapinduzi ya nne ya viwanda.

Akizungumzia malengo ya Mradi wa FoodLAND, Mkuu wa Mradi huo  kwa upande wa Tanzania Prof. Susan Nchimbi Msolla Kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo amesema unalenga hasa uboreshaji wa kilimo ili watu waweze kulima kilimo chenye tija na kinachohifadhi mazingira na kuzingatia lishe.

“ Tunalenga kuoanisha kati ya kilimo na lishe mara nyingi tumekuwa tukiona kwamba tunazalisha chakula kingi sana lakini wakati mwingine sehemu hizo hizo zinazozalisha chakula kingi lishe yao ni duni kwa hiyo sisi kwenye mradi huu tunataka tuweze kuoanisha uzalishaji wa chakula ili nchi yetu iwe na  watu wenye  lishe bora”, alisema Prof Msolla.

IMG 1559Mkuu wa Mradi wa FoodLAND  kwa upande wa Tanzania Prof. Susan Nchimbi Msolla Kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo akizungumzia malengo ya Mkutano huo.

Mtafiti huyo mkuu wa Mradi ameeleza kuwa matokeo ya Utafiti huo yatasaidia katika kuboresha na kushauri watu namna ya kulima, aina ya mazao ya kulima,kilimo cha aina gani kitumike na aina gani ya vyakula watu wale ili kuboresha afya zao .

Akieleza kwa ujumla malengo ya mradi ,utekelezaji wake mpaka sasa na Matarajio ya mbele Mratibu wa Mradi wa FoodLAND kwa nchi zote washiriki  Prof. Marco Setti kutoka Chuo Kikuu cha Bologna cha nchini Italy amesema mkutano huo ni fursa kubwa kwa washiriki wote kukutana pamoja na kubadilishana maarifa na mbinu za utekelezaji ili kufikia malengo tarajiwa.

Amesema kumekuwa na maendeleo makubwa na mazuri ya utafiti kwenye nchi zote wananchama kasoro Ethiopia ambako kuna kuchelewa kwa utekelezaji wa kazi mbalimbali kutokana na changamoto mbalimbali za nchi hiyo lakini wana Imani kuwa nao watakamilisha na kupata matokeo.

3 (4)

Mratibu wa Mradi wa FoodLAND kwa nchi zote washiriki Prof. Marco Setti kutoka Chuo Kikuu cha Bologna cha nchini Italy akieleza kwa ujumla malengo ya mradi, utekelezaji wake mpaka sasa na Matarajio ya mbele.

“Tayari tumeshazalisha takribani matokeo 30 na kuyawasilisha kwa wafadhili wetu  ambao umoja wa Ulaya (European Union) ambayo yanapatikana kwenye tovuti ya mradi na kwenye  tovuti ya Umoja wa Ulaya na kila mmoja anaweza kuyaangalia kujua kilichopatikana yapo mengine 7 yaliyozalishwa mwezi mmoja uliopita na mengine matano yanayohusu miongozo na zana za kufundishia yanaendelea kukamilishwa” alisema Prof. Seti.

 

IMG 1292Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano

Mradi wa FoodLAND ulianza kutekelezwa mwezi wa tisa mwaka 2020, ukishirikisha wadau 26 kutoka nchi 13 ambapo za Afrika inawakilishwa na Tanzania,Kenya,Uganda,Ethiopia, Tunisia, Morocco ambapo kwa mara ya kwanza wanakutana Tanzania kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa mradi huo baada ya miaka miwili yote kufanyika kwa njia ya mtandao kutokana na changamoto za ugonjwa wa UVIKO 19.

Na: Amina Hezron na Calvin Gwabara – Zanzibar.

Share this page