Nane nane 2022: Matukio mbalimbali katika picha

Maonesho ya kilimo, mifugo na uvuvi maarufu kwa jina la nane nane yaliyoanza rasmi Agosti 1 2022 yanaendelea katika viwanja vya Julius Nyerere (nane nane) mkoani Morogoro. 

Wageni mbalimbali wametembelea banda la Maonesho la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa ajili ya kujionea teknolojia mbalimbali zinazoonyeshwa na watafiti wa SUA kwa manufaa ya wakulima na wafugaji wa Tanzania.

Miongoni mwa wageni waliofika katika banda la SUA ni Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Raphael Chibunda, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam) Profesa Maulid Mwatawala na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa.

Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye maonesho hayo
 

SUA


Share this page