SUA mshindi wa tatu katika taarifa bora za fedha kitaifa

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, kimefanikiwa kuibuka Mshindi wa tatu katika Tuzo za Umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya mwaka 2020 (Best Presenter Financial Statements for the Year 2020 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na  Mashirika, ambazo hutolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) zilizofanyika siku ya Ijumaa tarehe 3 Disemba, 2021 kwnye Hotel ya APC Bunju Jijini Dar es Salaam.
 

SUA

Picha kubwa juu ni Mhasibu Mkuu wa Serikali ambaye   ndiye mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo  za Umahiri katika uandaaji wa taarifa za fedha ambazo hutolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) Bw. Leonard Mkude (kushoto) akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Dkt. Ibrahim Chikira Mjemah siku ya Ijumaa tarehe 3 Disemba, 2021 kwenye Hotel ya APC Bunju, Dar es Salaam. Picha inayofuata ni Dkt. Ibrahim Lubuwah akionesha tuzo hiyo mara baada ya kuipokea toka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Leonard Mkude (hayupo pichani),  akiwa sambamba na baadhi ya watumishi wengine wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo akiwemo Afisa Mkuu Fedha Bw. Peter Wilson Lubuwah (wa kwanza kushoto).

Share this page