SUA yawasilisha mchango wake kwa serikali

Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimetoa mchango wa  kiasi cha shilingi milioni 100 kwa Serikali katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 2019.

SUA

Hundi (Dummy cheque) hiyo imekabidhiwa na Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo SUA, Prof. Raphael Chibunda  kwa  Waziri wa fedha, Mhe. Philip Mpango kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage hazina jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kupokea hundi hiyo, Waziri Mpango amesisitiza Taasisi za Serikali kutoa gawio na mchango wao kwa Serikali kabla ya kufika tarehe 23 mwezi huu kama agizo la Mhe. Rais alilolitoa hivi karibuni wakati akipokea gawio la Taasisi na mashirika mbalimbali ya Serikali.
 

SUA


Mhe. Waziri amesema Serikali ina taasisi na mashirika 266 na hadi sasa mashirika  na taasisi 137 zimeshatoa gawio na michango kwa serikali yenye  jumla ya shilingi Trilioni 1.17 huku taasisi na mashirika 129 hayajawasilisha gawio wala mchango wowote kwa serikali.


 

Like & Share this page