Mafunzo ya ufugaji bora wa kuku kwa wafugaji 23 kutoka mikoa mbalimbali nchini, yamemalizika Novemba 20 katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, yakilenga kuongeza uzalishaji wa mayai na nyama pamoja na kuboresha lishe ya jamii.
Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Hilary Sagala ambaye ni Afisa Tawala amesema ufugaji bora wa kuku una mchango mkubwa katika kupunguza umasikini
Amesema watumishi wengi na wafanyakazi wa sekta binafsi wanapaswa kupata nafasi ya kujifunza ili hata wanapostaafu waweze kuwa na shughuli za kukuza uchumi wao na kupunguza umaskini katika Kaya.

Ufugaji wa kuku una mchango katika kuondoa umaskini