Wakulima nchini wametakiwa kufuata kanuni na taratibu bora za kilimo ikiwa ni pamoja na kujua afya za mashamba yao kabla ya kuanza kulima ili waweze kupata mavuno yenye tija.
Ushauri huo umetolewa na Mtaalamu wa Maabara ya Udongo kutoka Ndaki ya Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo na Jiolojia wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Bw. Stevenson Pelegy Noah wakati akizungumza na SUAMEDIA katika Maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika jijini Dar Es Salaam.