Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kinawakaribisha vijana wenye umri wa miaka 18-35 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kushiriki katika mafunzo ya ujuzi wa kidijitali yatakayolenga kuongeza uwezo wa vijana katika ajira na ujasiriamali.
SIFA ZA MUOMBAJI
1. Vijana wenye umri wa miaka 18-35 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
2. Wajasiriamali vijana na wamiliki wa biashara ndogo.
3. Awe na uwezo wa kutumia kompyuta mpakato, tablet au simu janja.
4. Kitambulisho halali (ZanID, NIDA au Kitambulisho cha Mpiga Kura).
5. Uthibitisho wa makazi.
6. Majina kamili, jinsia na umri.
7. Taarifa za taasisi/shirika na biashara, pale inapohusika.
MAF UNZO NI BURE!!! Mafunzo haya hayana ada na yanafadhiliwa kupitia Mradi wa HEET (Higher Education for Economic Transformation).
MWISHO WA MAOMBI: 15 Septemba 2026
Omba Mtandaoni: https://shorturl.at/Ij1iL
Mahali: Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
Tarehe: 21 - 26 Sept 2026
Muda: Saa 02-10:00 jioni
Ardhi ni Hazina