TAZAMA:Mdahalo wa kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine-27/5/2021


​​​​​​​Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kiliandaa wiki ya kumbukizi ya hayati Edward Moringe Sokoine kuanzia tarehe 24 hadi 27 mwezi mei mwaka 2021, Lengo likiwa ni kumuenzi aliyekuwa mmoja wa viongozi shupavu, mzalendo na mchapakazi katika taifa la Tanzania, hayati Edward Moringe Sokoine,ambaye mchango wake kwenye maendeleo ya sekta ya Kilimo hapa nchini pamoja na uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) havitasahaulika


Shughuli mbalimbali zilifanyika kwenye wiki ya kumbukizi ya hayati Sokoine ikiwemo maonesho ya teknolojia na bunifu mbalimbali, mkutano wa kisayansi pamoja na mdahalo wa kitaifa uliofanyika siku ya tarehe 27/5/2021 ambapo mada zilizojadiliwa zilikuwa zinaendana na kauli mbiu yam waka huu ambayo ni Teknolojia za kilimo Kuzalisha kwa tija na ushindani katika soko la Tanzania kuelekea uchumi wa kati wa juu.

 

SUA

​​​​​​​

Like & Share this page