Ufaransa Kuimarisha Ushirikiano na SUA

Katika kuhakikisha ushirikiano baina Tanzania na Ufaransa unaimarika Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania HE Nabil Hajlaoui amefanya ziara katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ili kujua maeneo ya kimkakati ambayo Ufaransa inaweza kushirikiana na Chuo.

 

Ufaransa Kuimarisha Ushirikiano na SUA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda (kulia) akimkaribisha Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania HE Nabil Hajlaoui

Hayo yamebainishwa Februari 6, 2023 mkoani Morogoro na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Esron Karimuribo, wakati wa ziara ya Balozi huyo katika Chuo Kikuu cha Sokoine.

Amesema ujio wa Balozi huyo wa Ufaransa SUA ni wa baraka kwani umekuwa na matokeo mazuri zaidi katika kusikiliza mawazo ya kibiashara kutoka kwa vikundi na makampuni ya wanafunzi chuoni hapo ambapo amewahakikishia kuwaunga mkono na kuahidi kuwatafutia soko kutokana na bidhaa wanazozalisha.

IMG 0752.CR2

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania HE Nabil Hajlaoui (katikati) akiendesha majadiliano katika ukumbi wa Baraza wa SUA, (kushoto) ni Prof. Karimuribo

Prof. Karimuribo amesema matokeo mengine ni kwamba kwa wale ambao wametoa mawazo mazuri kupitia Mradi wa ’Innoversity’ Balozi ameyapenda hivyo ameyapa baraka na wanategemea kuwa hatua inayofuata ni kuyachanganua ili wapate wanafunzi ambao wataenda nchini Ufaransa kati ya mwezi wa Nne na wa Sita, 2023 kwa ajili ya kujifunza ili watakaporudi waweze kuendeleza mawazo yao kibiashara.

“Kuna kundi la wale ambao wanatengeneza au kufanya Samaki kama mapambo majumbani hata maofisini Balozi amesema yuko tayari kuhakikisha anayaunga mkono na jambo zuri ni kuwa tumebahatika tu kwamba kupitia Programu ya STEPS ya SUA ambayo inawasaidia na kuwahamasisha wanafunzi wajiunge halafu wasajili Makampuni yao ya kibiashara wakati wakiendelea na masomo sasa kupitia uhamilishaji huo kumechangia kwa kiasi kikubwa hata kupata mawazo mazuri”, amesema Prof Karimuribo

IMG 0767.CR2

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania HE Nabil Hajlaoui (wa pili kushoto) akikagua moja ya majengo yaliyoko SUA, (mbele aliyevaa Kaunda Suti) ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Maulid Mwatawala

Amesema wapo wengine ambao wanatengeneza Unga wa Mchicha (AMARATH) wenye Madini ya kutosha, Vitamini ya kutosha kwa ajili ya kuwasaidia kinamama wajawazito pamoja na watoto wenye Utapiamlo hawa nao wazo lao litaboreshwa Zaidi.

Prof. Karimuribo ameongeza kuwa SUA ni Taasisi ambayo inatoa Taaluma lakini kwao kama Chuo wanaona ni matokeo mazuri kwa kuwa kupitia ushirikianao huo wale wanafunzi ambao wanawafundisha wanatoka chuoni hapo wakiwa tayari ni wajasiliamali na wana makampuni yao hivyo hawatategemea kuajiriwa nao kutoa fursa za ajira kwa wengine.

IMG 0801.CR2

IMG 0789.CR2

 Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania HE Nabil Hajlaoui (kulia) akiangalia matunda aina ya Zabibu yanayolimwa kwa majaribio katika Shamba na Mafunzo la SUA mkoani Morogoro, (kushoto picha ya juu)  Mkuu wa Idara ya Shamba la Mafunzo SUA Dkt. Newton Kilasi 

 

Na; Winfrida Nicolaus

Picha zote na Gerald Lwomile

Share this page