Uzinduzi Wa Kumbukizi Ya 18 Ya Hayati EDWARD MORINGE SOKOINE Mei 2023

Katika kukuza soko la nyama hapa nchini Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesema inadhamira ya kufanya kampeni ya kuchanja mifugo kwa kufuata kalenda ili kuongeza soko la nyama nje ya nchi kutoka tani 12 ya sasa hadi tani 100.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb)  Mjini Morogoro  wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya kumbukizi ya 18 ya Hayati Edward Moringe Sokoine yanayo fanyika Kampasi Kuu ya Edward Moringe Sokoine .

Uzinduzi Wa Kumbukizi Ya 18 Ya Hayati EDWARD MORINGE SOKOINE Mei 2023

Amesema licha ya wafugaji kuchanja mifugo yao, bado zoezi hilo haliratibiwi ipasavyo hivyo kufanya baadhi ya nchi kushindwa kununua nyama hapa nchini kwa sababu ya kutochanja mifugo.

 

“Wachina wanataka nyama yetu, lakini wanaiogopa, wanasema inamaradhi, kwa sababu hatuchanji, si kweli, kwamba watu hawachanji kabisa, yawezekana watu wanachanja kule kwenye Halmashauri, lakini hakuna utaratibu wenye kueleweka.” Amesema Waziri Ulega.

Pia Waziri Ulega amesema, kuanzishwa kwa kampeni hiyo kutatoa fursa kwa wanafunzi wanaosoma Shahada za  Mifugo ikiwemo wanaotoka  SUA kujifunza kwa vitendo na kwamba kutaongeza ajira kwa vijana wengi wanaomaliza Elimu ya Juu  hapa nchini.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda, amesema katika kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine, SUA kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi, wapo katika hatua za mwisho za kuandika kitabua, cha kumbukumbu  ya Hayati Sokoine. 

“Chuo chetu kwa kushirikina na Taasisi ya Uongozi tupo katika hatua za mwisho za kukamirisha uandishi wa kitabu hicho, kwahiyo kitakapokuwa tayari, tumekubaliana na wenzetu wa uongozi, tutalifanya liwe tukio kubwa  la uzinduzi wa hicho kitabu.” Alisema Prof. Chibunda.

WhatsApp Image 2023-05-24 at 10.41.44 AM

Amesema kwa mwaka huu 2023 SUA itaadhimisha kumbukizi ya Sokoine kuanzia Mei 23 hadi 26 kwa kufanya shughuli mbalimbali kama kufanya mkutano wa Kisayansi kwaajili ya wanataaluma, watafiti, wanafunzi na wadau.

Kwa mwaka 2023 maadhimisho hayo yanabebwa na Kauli mbiu isemayo, Mazingira wezeshi  kwa vijana kushiriki katika  Kilimo, sera , miongozo na utendaji, ambapo kauli hiyo  inalenga kuhamasisha vijana  kushiriki kikamilifu  katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi  kwa kuwawekea mazingira rafiki.

WhatsApp Image 2023-05-24 at 10.41.39 AM (1)

WhatsApp Image 2023-05-24 at 10.41.45 AM

WhatsApp Image 2023-05-24 at 10.41.41 AM

Share this page