ANGALIA: Kongamano la Safari ya Kilimo Katika Miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika

Kwa niaba ya Menejimenti nampenda kuwataarifu kuwa siku ya Ijumaa tarehe 06 Desemba, 2024 kuanzia saa 8:00 mchana katika Ukumbi wa Multipurpose, Kampasi ya Edward Moringe, Morogoro tutakuwa na Kongamano la Miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika. Mada Kuu katika Kongamano hilo ni:- Kilimo chetu, tulipotoka tulipo na mustakabali wa Tanzania bora Uwekezaji kwenye Kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi Kilimo biashara na mbinu za kisasa kuelekea mapinduzi ya nne ya viwanda Kilimo cha kisasa, ushiriki wa vijana na hatma ya mageuzi ya uchumi wa nchi Maono na uthabiti wa serikali ya awamu ya sita katika kuibua fursa mpya katika kilimo Miongoni mwa watoa mada katika Kongamano hilo ni pamoja na Bw. Husein Omar Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Prof. Daniel Ndyetabura, Mhadhiri SUA, Bi. Yasinta Nzogela, Mhadhiri SUA na Bw. Juma Haji, Afisa Mwandamizi, Uvuvi wa Bahari Kuu. Karibuni tushiriki bila kukosa.

Tanzia

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Prof. Raphael Chibunda, anasikitika kutangaza kifo cha Mfanyakazi Mwenzetu Prof. Benedicto B. Kazuzuru wa Idara ya Hisabati na Takwimu aliyefariki Dunia tarehe 03.12.2024 katika hospitali ya Mloganzila alikokuwa akipatiwa matibabu. Mwili wa marehemu utaagwa tarehe 06.12.2024 Dar es salaam na kusafirishwa kuja Morogoro. Msiba upo nyumbani kwake Idiva karibu na shule ya Msingi “Holy Cross”, ambapo mazishi yatafanyika Jumamosi tarehe 07.12.2024 hapa Morogoro katika makaburi ya Kola. Tuungane kwa pamoja kuifariji familia ya marehemu katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao. Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe, Amina