Kupitia Serikali ya Awamu ya Tano, Chuo kimetatua changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujenga Maabara Mtambuka Kampasi Kuu, Maabara ya Sayansi Solomon Mahlangu, kukarabati viwanja vya
michezo, kuanzisha shamba la mafunzo la mfano, kukarabati Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Wanyama, kukarabati madarasa na mabweni, kununua mabasi, pamoja na kupanua na kusajili Hospitali ya SUA.
Maboresho hayo ya miundombinu yamekifanya Chuo kuongeza programu mpya za masomo 26, kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 9,165 mwaka wa masomo 2015/16 hadi 13,199 mwaka wa masomo
2019/20. Katika kipindi hiki jumla ya wataalamu 13,178 ambao wamehitimu katika program mbalimbali.