TANGAZO LA MAFUNZO YA UFUGAJI BORA WA KUKU KWA MUDA MFUPI (WIKI MOJA)

Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) kwa niaba ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) inapenda kuwatangazia kuwa, kutakuwa na mafunzo ya muda mfupi (wiki moja) ya ufugaji bora wa kuku. Mafunzo hayo yatafanyika katika Ukumbi wa Giraffe uliopo katika Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) Kampasi ya Edward Moringe – SUA, Morogoro kuanzia tarehe 29.01.2024 hadi 01.02.2024. Walengwa, idadi ya waombaji na idara itakayotoa mada imeoneshwa kwenye Kielelezo Na. 1.

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo katika utekelezaji wa programu ya kushirikisha vijana katika kilimo ya Jenga Kesho Iliyo bora (Building a Better tomorrow- BBT) wanawaarifu Waombaji wa nafasi za ajira za muda kupitia program maalum ya kuendeleza zao la Pamba nchini zilizotangazwa tarehe 12.12.2023, kuwa wanaitwa kwenye usaili katika Kampasi ya Edward Moringe Mjini Morogoro, kama ifuatavyo: