Uzinduzi Wa Kumbukizi Ya 18 Ya Hayati EDWARD MORINGE SOKOINE Mei 2023

Katika kukuza soko la nyama hapa nchini Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesema inadhamira ya kufanya kampeni ya kuchanja mifugo kwa kufuata kalenda ili kuongeza soko la nyama nje ya nchi kutoka tani 12 ya sasa hadi tani 100. Hayo yameelezwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb)  Mjini Morogoro  wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya kumbukizi ya 18 ya Hayati Edward Moringe Sokoine yanayo fanyika Kampasi Kuu ya Edward Moringe Sokoine .