Tazama Video: Mafanikio Ya Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)

Chuo kimejiwekea malengo ya kimkakati ambayo ni kuongeza udahili wa wanafunzi, miradi ya utafiti na kuboresha huduma za ugani na ushauri wa kitaalamu. Hata hivyo kwa miaka mingi Chuo kilishindwa kufikia malengo hayo kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo uchakavu wa miundombinu na mifumo ya huduma za jamii.