SUA Yazindua Dawati la Jinsia

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimezindua Dawati la Jinsia chuoni hapo ili kutimiza malengo ya serikali ya kupunguza na kutokomeza kabisa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii hususani kwenye Vyuo Vikuu nchini.  Dawati hilo limezinduliwa tarehe 10 Oktoba, 2023 Kampasi Kuu ya Edward Moringe na Prof. Samwel Kabote  aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo akimwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda ambapo amesema atafurahi kuona Dawati hilo likiwa chachu ya kuimarisha maendeleo ya Jinsia katika maeneo yanayozunguka Chuo chao.