SUA anzisheni Kanzidata ya wanafunzi waliofaulu vizuri - Dkt. Francis Michael
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt Francis Michael ameshauri vyuo vikuu nchini kuwa na Kanzidata maalumu kwa ajili ya wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao ili zinapotoka nafasi za ajira kwenye taasisi mbalimbali waweze kupewa kipaumbele katika ajira.