SUA kukarabati Jengo lililomilikiwa na Wajerumani ili kutumika kwa shughuli za Utalii, Mafunzo kwa Wanafunzi wa Shahada ya Utalii

Katika kuhakikisha Sekta ya Utalii inakua na kuleta tija hapa nchini, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kupitia Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii pamoja na Kurugenzi ya Miliki na Kazi kimeweza kukagua ukarabati wa jengo lililopo eneo la Morning Sight katika Safu ya Milima ya Uluguru. Jengo hili hutumika kwa shughuli za utalii.

Wahitimu 3,744 wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo watunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu ya Chuo Kikuu

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba (wa pili waliokaa ) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman (wa tatu kulia waliokaa) na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda (wa kwanza kulia waliokaa) na viongozi mbalimbali na wanataaluma wa chuo hicho.