Wanafunzi waonesha ubunifu wa mavazi mbalimbali
Katika maonesho hayo, wanafunzi wa mwaka wa pili wanaosoma somo la (Cultural Aspects of Clothing) walibuni na kutengeneza mavazi mbalimbali kulingana na makabila na tamaduni za hapa Tanzania. Wanafunzi wa mwaka wa tatu kupitia somo la (Costume Design) walitengeneza mavazi mbalimbali yanayovaliwa kwenye matukio na shughuli mbalimbali kwa kutumia vitu vya gharama nafuu vinavyopatikana katika mazingira yetu (Locally available cheap materials).