CCM Yaipongeza SUA kwa Utekelezaji wa Miradi kwa Vitendo

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amekipongeza Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa utekelezaji wa Miradi kwa vitendo na kuwataka kuanzisha mfumo mzuri utakaowezesha kupata vijana ambao hawafikirii kuajiriwa bali kujiajiri ili waajiri wengine kwa kuwa ndiyo njia pekee ya kulifanya Taifa kufikia malengo yake ya kumkwamua mwananchi wa kawaida ambaye maisha yake yanategemea Kilimo.

Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Prof. Raphael Chibunda, anapenda kuwataarifu kuwa, kutakuwa na ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo siku ya Jumapili tarehe 5 Januari, 2023 kuanzia saa 3:00 Asubuhi.