Tanzania Inapoteza Zaidi ya Shilingi Bilioni 19 Kutokana na Athari za Minyoo Tegu ya Nguruwe

Tafiti zimeonesha kuwa, kwa mwaka mmoja Tanzania inapoteza zaidi ya shilingi bilioni 19 kutokana na athari zinazotokana na Minyoo tegu ya Nguruwe kwa jamii ikiwemo matibabu na kutupa nyama yenye maambukizi Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mtandao wa Kisayansi CYSTINET Africa Prof. Helena Ngowi kwenye Warsha ya kujadili mrejesho wa matokeo ya Utafiti kuhusu namna ya kudhibiti Mnyoo Tegu ya Nguruwe Tanzania iliyofanyika Jijini Dodoma.

Mradi wa Cystnet Afrika Wawasilisha Matokeo ya Utafiti wa Minyoo Tegu ya Nguruwe Tanzania

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu NIMR, wamefanya utafiti na kuja na mapendekezo yatakayowezesha kumaliza tatizo la minyoo tegu ya Nguruwe ambayo ina madhara makubwa kwa afya ya Binadamu na Wanyama.