Matokeo ya Utafiti ya Mradi wa FoodLAND Kusaidia Kuboresha Kilimo na Lishe Afrika.
Imeelezwa kuwa matokeo yote mazuri ya Mradi wa Chakula Kilimo na Lishe (FOODLAND) yaliyopatikana kwenye nchi zinazotekeleza mradi huo yatakwenda kuisaidia jamii katika kuhusanisha Kilimo, Matumzi ya mazao ya chakula na lishe na hivyo kupunguza changamoto za chakula na lishe Afrika.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala wakati akifungua Mkutano Mkuu wa wa tatu wa Mwaka wa Mradi huo uliofanyika visiwani Zanzibar wa kufanya tathimini ya kazi zilizofanyika ndani ya mradi ili kuendelea kuboresha ufanyaji kazi wa mradi huo.