Tanzania Inapoteza Zaidi ya Shilingi Bilioni 19 Kutokana na Athari za Minyoo Tegu ya Nguruwe
Tafiti zimeonesha kuwa, kwa mwaka mmoja Tanzania inapoteza zaidi ya shilingi bilioni 19 kutokana na athari zinazotokana na Minyoo tegu ya Nguruwe kwa jamii ikiwemo matibabu na kutupa nyama yenye maambukizi
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mtandao wa Kisayansi CYSTINET Africa Prof. Helena Ngowi kwenye Warsha ya kujadili mrejesho wa matokeo ya Utafiti kuhusu namna ya kudhibiti Mnyoo Tegu ya Nguruwe Tanzania iliyofanyika Jijini Dodoma.