Walimu na Wanafunzi Kampasi ya SUA Mizengo Pinda Wafurahia Mafunzo ya Jinsia
Wanataaluma na Wanafunzi katika Kampasi ya SUA Mizengo Pinda Mkoani Katavi wameupongeza Mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET) kwa kuwezesha na kuhimiza elimu ya masuala ya Jinsia katika Taasisi za Elimu Chuoni kwakuwa inasaidia kufanya mazingira ya Chuo kuwa salama kwa wote.