Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Misitu, Wanyapori na Utalii SUA washiriki zoezi la usafi chuoni
Katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama kwa viumbe hai pamoja na jamii, wanafunzi wanaosoma Shahada kutoka Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wameaswa kushiriki katika zoezi la kufanya usafi kwani jambo hilo ni endelevu na litawasaidia katika masomo yao na hata baada ya kuhitimu.