SUA Yasaini Mkataba wa Ushirikiano na Taasisi 7 za Wizara ya Kilimo

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimesaini Mkataba wa Ushirikiano na Taasisi 7 za Wizara ya Kilimo wenye lengo la kukuza uchumi wa Nchi kupitia Sekta ya Kilimo.  Zoezi hilo limefanyika Februari 9, 2023 katika Kampasi ya Edward Moringe Sokoine mkoani Morogoro ambapo limeongozwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo cha SUA, Prof. Raphael Chibunda.