Matumizi ya Matandazo katika Kilimo kwa wakulima wa zao la Maharage
Katika kuhakikisha wakulima wanakabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia mradi wa FOODLAND waliandaa na kutoa mafunzo ya namna ya kutumia Matandazo katika Kilimo hususan kwa wakulima wa zao la Maharage kutoka Kijiji cha Ndole Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.